0
Timu ya soka ya Kagera Sugar imefanikiwa
kuichapa timu ya Simba kwa jumla ya bao 2-1
katika mchezo wa ligi kuu bara ambapo baadhi ya
wachambuzi wa soka wamesema kuwa kutokana
na Kagera Sugar kuifunga Simba inawezekana
ikawa ndiyo nafasi kwa yanga kutetea ubingwa
wao ambapo baada ya mchezo wa leo Simba
wamebaki na pointi zao 55 huku Yanga wakijikita
kileleni wakiwa na pointi 56 baada ya michezo
25.
katika mchezo huo uliopigwa kwenye dimba la
Kaitaba ulishuhudia timu ya soka ya Simba
wakishindwa kutumia nafasi zao vyema walizopata
na kujikuta wakifungwa bao 2-1 ambapo mabao
ya Kagera Sugar yalifungwa na Mbaraka Yusuph
Huku bao la pili likifungwa na Edward Christopher
huku bao la kufutia machozi kwa Simba sports
Club likifungwa na Mzamilu Yasin dakika 61 ya
kipindi cha pili.
Kwa matokoe hayo yanga wanaendelea kuwa
kileleni mwa ligi hiyo wakiwa na jumla ya pointi
56 wakifuatiw ana Simba wenye pointi 55 huku
Kagera Sugar wakifikisha jumla ya pointi 45 huku
nafasi ya nne ikishikwa na Azam wenye pointi 44.

Chapisha Maoni

 
Top