vijana chini ya umri wa
miaka 17, Serengeti Boys
imelazimishwa sare ya
kufungana mabao 2-2 na
Ghana katika mchezo wa
kirafiki uliofanyika Uwanja wa
Taifa, Dar es Salaam jioni ya
leo.
Huo ulikuwa mchezo wa tatu
wa majaribio katika
maandalizi ya Serengeti Boys
kwenda Gabon kwenye fainali
za Afrika za U-17 mwezi Mei
baada ya awali kuifunga
Burundi 3-0 na 2-0 mjini
Bukoba wiki iliyopita.
Ghana walitangulia kwa
mabao mawili ya Sulley
Ibrahimu dakika ya 30 na
Arko Mensah dakika ya 73,
kabla ya Tanzania
kusawazisha kupitia kwa
Asad Juma kwa penalti na
Muhsin Malima mabao yote
yakifungwa dakika za
nyongeza baada ya kutimu
dakika 90 za kawaida za
mchezo.
Beki wa Ghana, Yusif
Abdulrazak akibinuka
kuondosha mpira kwenye
himaya ya Yohana Nkomola
wa Tanzania leo
Mapema kabla ya mchezo
huo, Waziri wa Habari
Utamaduni Sanaa na
Michezo, Dk. Harrison
Mwakyembe aliwakabidhi
Serengeti Boys bendera
tayari kwa safari ya Morocco
Jumatano kwenda kuweka
kambi ya mwezi mmoja
kujiandaa na fainali za
AFCON U-17 nchini Gabon.
Kikosi cha Tanzania;
Ramadhani Kabwili, Ally
Msengi, Israel Mwenda,
Nickson Kibabage, Dickson
Job, Ally Ng'anzi, Asad Juma,
Shaaban Zubeiry, Yohana
Nkomola, Kevin Naftal na
Abdallah Rashid.
Ghana; Ibrahim Danlad, Ayiah
Eric, Yakubu Najeeb,
Alhassan Rashid, Osman
Faisal, Yusif Abdulrazak,
Owusu Bismarck Terry, Antwi
Nana Kamwe, Levesh Gabriel,
Sulley Ibrahim na Toku
Emmanuel.
Chapisha Maoni