0
Mashetani wekundu wa Old Trafford klabu ya
Manchester United imebanwa nyumbani na
kulazimishwa sare ya bila kufungana na wageni
West Brom Albion.
Licha ya kutawala kwa kiwango kikubwa katika
mchezo wa leo lakini kukosekana kwa Zlatan
Ibrahimovic pengine kunaweza kuelezwa kama ni
moja ya sababu za kushindwa kupata goli baada
ya Zlatan kuongoza katika orodha ya wafungaji
bora wa United msimu huu.
Hii ni sare ya 8 nyumbani kwa Manchester United
msimu huu na kufanya harakati zao za kutinga
katika Top 4 kuzidi kuwa ngumu
United sasa imefikisha pointi 53 katika nafasi ya 5.

Chapisha Maoni

 
Top