Juventus imeichapa Monaco kwa mabao 2-0 katika mechi ya kwanza ya nusu fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya dhidi yao kwenye Uwanja wa Stade de Louis mjini Monaco.
Mshambuliaji nyoya wa Monaco, Kylian Mbappe hakuweza kuonyesha cheche zake kama ilivyotarajiwa.
Mabao yote ya Juve yamefungwa na
mkongwe Gonzalo Higuain na kuweka rekodi ya Monaco kupotea mechi ya kwanza katika Ligi ya Mabingwa Ulaya msimu huu.
Kabla ya hapo, Monaco haikuwa imepoteza mechi yoyote nyumbani tokea Desemba, mwaka jana.
Monaco starting XI: Subasic, Fabinho, Glik, Jemerson, Sidibe, Dirar, Bernardo Silva (Toure), Bakayoko (Moutinho), Lemar
(Germain), Falcao, Mbappe
Juventus starting XI: Buffon, Barzagli, Bonucci, Chiellini, Dani Alves, Marchisio (Rincon), Pjanic, Alex Sandro, Higuain (Cuadrado), Dybala, Mandzukic
Juventus subs: Benatia, Lemina, Asamoah, Neto, Lichtsteiner
Chapisha Maoni