0
Uongozi wa klabu ya Simba Sports
imeamua kuliburuza Shirikisho la
Soka nchini 'TFF' katika mahakama ya
usuluhishi ya Michezo Duniani 'CAS'.
Hatua hiyo inakuja ikiwa ni Njia ya
Kutafuta haki yao kufuatia suala la
kupokwa pointi tatu baada Kagera
Sugar kumchezesha mchezaji mwenye
kadi tatu za njano.
Rais wa klabu hiyo Evans Aveva
amesema kuwa sababu tatu
zilizotolewa na Kamati ya Katiba
Sheria na Hadhi za Wachezaji
hazikuwa na mashiko kwani suala la
mchezaji kucheza akiwa na kadi tatu
ni kosa kwa mujibu wa kanuni.
Tunaonewa.
Aidha Aveva amewaambia waandishi
wa habari katika makao makuu ya
klabu hiyo kuwa Simba imekuwa
ikionewa na TFF kutokana na
maamuzi mbalimbali yanayotolewa
ndiyo maana wakaamua kupeleka
malalamiko yao FIFA.
Simba ina subiri kupewa barua na TFF
inayoonesha kupokwa pointi hizo ili
kuweza kupeleka malalamiko yao CAS
kwa ajili ya kupata alama hizo
ambazo wanasema ni halali kwao.
-Tunasubiri barua maalumu ya
kupokwa pointi zetu ili twende FIFA
na ikibidi kwenye mahakama ya
usuluhishi 'CAS' Ni kosa kikanuni
mchezaji kucheza akiwa na kadi tatu
za njano" Aveva Alisema.

Chapisha Maoni

 
Top