0
Kocha Mrundi anayeinoa Mbao Fc ya
Jijini Mwanza, Etienne Ndairagije
amesema sasa Benchi la Ufundi la
Timu hiyo linaweka mawazo katika
Mchezo wa ligi dhidi ya Yanga kwani
ndio mchezo pekee ambao unaweza
kuwabakisha katika Ligi Kuu soka
Tanzania Bara.
Ndairagije ameyasema hayo wakati
akizungumza na Mtandao huu mara
baada ya Mchezo wa ligi dhidi ya
Kagera Sugar ambao Ulifanyika katika
Uwanja wa Kaitaba na kushuhudia
Mbao FC wakichezea kichapo cha
Mabao 2-1.
Ndairagije amesema Mara baada ya
kupata matokeo hayo ambayo ni
Sehemu ya mchezo sasa wanaelekeza
nguvu zao katika mchezo ujao na wa
mwisho dhidi ya Yanga mchezo
ambao ameutaja ni wa muhimu zaidi.
-Ndugu zetu Kagera walijituma na
Kujitahidi ndio maana wakaibuka na
ushindi katika mchezo huu, kwa sasa
tunaelekeza nguvu zetu kwenye
mchezo dhidi ya Yanga ambao ndio
upo mbele yetu, tutaangalia namna ya
kuweza kushinda ili tubaki kwenye
ligi’ Alisema Ndairagije.
Msimamo.
Mbao ambao walipoteza mchezo wa
16 baada ya kufungwa na Kagera
Sugar wapo katika hatari ya kushuka
daraja kwani sasa wapo katika nafasi
ya 13 wakiwa na alama 30, ambapo
kama watapoteza dhidi ya Yanga
watasubiri matokeo ya Timu nyingine.

Chapisha Maoni

 
Top