Msuva, anatarajiwa kukosa mchezo wa Jumanne dhidi ya Toto Afrika, baada ya kupasuka na kushonwa nyuzi nne kwenye mchezo dhidi ya
Mbeya City
Kinara wa mabao kwenye ligi ya Vodacom, Simon Msuva, anatarajiwa kukosa mchezo wa Jumanne dhidi ya Toto Afrika, baada ya kupasuka na kushonwa nyuzi nne kwenye mchezo wa jana dhidi ya Mbeya City.
Daktari wa Yanga Edward Bavu, ameisema kuwa,
Msuva anaweza kuikosa mechi hiyo kutokana na ukaribu wa mechi zilizokwa sasa huku akisema
wataendelea kuangalia hali yake hadi kufikia siku ya mchezo.
“Amepasuka na tumemshona nyuzi nne, kuhusu kucheza itategemea na maendelea ya kidonda hadi kufikia siku ya mchezo lakini uwezekano
unaweza kuwa mdogo kutokana na mechi kupangwa karibu karibu,”amesema Bavu.
Daktari huyo amesema kama mchezo huo ungekuwa Jumatano angalau Msuva angekuwa na nafasi kubwa ya kucheza lakini kwa Jumanne nvigumu hadi watakapoona maendeleo ya
kidonda siku ya mchezo.
Kwa upande wake Msuva, amesema anatamani kupona haraka ili aweze kurejea uwanjani Jumanne na kuipigania timu yake kupata ushindi
ambao utawasaidia kutetea taji lao la Vodacom kwa msimu wa tatu sasa.
Msuva amesema ameumia lakini hakuna wa kumlaumu kwasababu mambo kama hayo hutokea kwenye soka hivyo amewashukuru
wachezaji wenzake kwa kupambana na kuhakikisha wanashinda mchezo huo uliokuwa mgumu.
Bao alilofunga Msuva lilikuwa la 14 msimu huu na kumweka katika nafasi nzuri ya kutetea kurudia mafanikio aliyoyapata msimu wa 2014/15 alipokuwa mfungaji bora kwa kufunga mabao 17 na Amissi Tambwe kushika nafasi ya pili akiwa
na mabao 14.
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni (Atom)
Chapisha Maoni