0
Michuano ya 12 ya Mataifa Afrika kwa
vijana chini ya Umri wa Miaka 17,
inayosimamiwa na Shirikisho la soka
Afrika CAF, imefunguliwa rasmi
Jumapili Mei 14 katika Uwanja wa
Stade de Port Gentil uliopo Mjini Port
Gentil nchini Gabon.
Mashindano hayo ambayo
yanahusisha vijana waliochini ya Umri
wa miaka 17, yanashirikisha Jumla ya
Timu nane kutoka Nchi Nane ambazo
ni wanachama wa CAF, huku miji
mitatu ya nchini Gabon ikitarajiwa
kutumika katika Michuano hiyo.
Timu ya Taifa ya Tanzania ‘Serengeti
Boys’ ni mojawapo ya Timu ambazo
zinashiriki katika Mashindano hayo
ambapo imepata nafasi hiyo baada ya
Timu ya Taifa ya Kongo Brazzaville
kutolewa mashindanoni baada ya
kugundulika kuwa walimtumia
mchezaji Langa-Lesse Bercy aliyezidi
umri.
Kundi B.
Serengeti boys wamepangwa katika
kundi B pamoja na Timu za Mali,
Angola na Niger ambapo watafungua
Dimba Jumatatu kwa kucheza na Mali
kabla ya Kukutana na Angola Mei 18
na Kumaliza na Niger Mei 21.
Ikumbukwe kwanza Timu nne
zitakazofanikiwa kufuzu katika hatua
ya Nusu Fainali zitafuzu moja kwa
moja Katika mashindano ya Kombe la
Dunia kwa vijana wa umri huo,
Mashindano ambayo yanatarajiwa
kufanyika India kuanzia Oktoba 6 hadi
28.

Chapisha Maoni

 
Top