0
Kikosi cha wachezaji 18 na Viongozi 9 wa Timu ya Taifa ya Soka ya Rwanda 'Amavubi' kimeanza safari ya kuelekea Jijini Mwanza kucheza mchezo wa Kufuzu kwa fainali za Mataifa Afrika kwa wanaocheza ligi za Ndani 'CHAN'.
Kikosi hicho kimeanza safari Usiku huu na Shirika la Ndege la Rwanda Air ambapo watatua Jijini Dar es Salaam Kabla ya kuunganisha moja kwa moja Jijini Mwanza.
Amavubi watacheza mchezo wao Jumamosi ya Julai 15 katika Uwanja wa CCM Kirumba na Timu ya Taifa ya Soka ya Tanzania 'Taifa Stars' na Kabla ya kurudiana tena Juma moja baadae Jijini Kigali.
Wachezaji 18.
Kikosi kinachotarajiwa kusafiri ni pamoja na Walinda milango Ndayishimiye Eric (Rayon Sports Fc) na Nzarora Marcel (Police Fc) huku mabeki wakiwa ni Nsabimana Aimable (APR Fc), Manzi Thierry (Rayon Sports Fc), Kayumba Soter (AS Kigali), Rucogoza Aimable (Bugesera Fc), Bishira Latif (AS Kigali), Imanishimwe Emmanuel (APR Fc), Muvandimwe Jean Marie Vianney (Police Fc) na Iradukunda Eric (AS Kigali).
Viungo ni Niyonzima Olivier (RAyon Sports Fc), Mukunzi Yannick (APR Fc), Bizimana Djihad (APR Fc), Muhire Kevin (Rayon Sports Fc) na Nshuti Savio Dominique (AS Kigali), Huku washambuliaji ni Mico Justin (Police Fc), Nshuti Innocent (APR Fc) na Mubumbyi Barnabe (AS Kigali).

Chapisha Maoni

 
Top