0
Kesi ya madai ya utakakatishaji fedha inayowakabili viongozi wa Simba, Mwenyekiti Evance Aveva na Makamu Mwenyekiti Godfrey Nyange Kaburu imetajwa kwa mara ya tatu leo (Julai 13) katika mahakama ya hakimu mkazi Kisutu.
Aveva na Kaburu wanakabiliwa na tuhuma za kughushi nyaraka za klabu ya Simba na kutakatisha dola 300,000 (zaidi ya 650 Milioni) na wamekuwa rumande tangu Juni 29 mwaka huu.
Upande wa mashtaka unaoongozwa na wakili wa Takukuru uliomba mahakama kesi hiyo isikilizwe Julai 20 kwa kuwa upelelezi bado haujakamilika.
Hakimu Mkazi Mwandamizi, Victoria Nongwa aliliridhia ombi la mawakili wa Takukuru na kuwataka kufanya hima kukamilisha upelelezi.
"Hizi ni kesi zisizokuwa na dhamana na lazima washakiwa wapate haki zao, fanyeni hima upelelezi ukamilike hadi Julai 20,"alisema
Wanachama Simba wamiminika Kisutu
Kabla ya kesi hiyo kutajwa wanachama wa Simba walianza kufika mahakamani mapema ili kujua hatima ya viongozi wao.
Baadhi ya waliofika ni mgombea wa nafasi ya makamu wa rais katika uchaguzi mkuu wa TFF, Mulamu Ng'ambi, mwenyekiti wa zamani wa Simba, Hassan Dalali na mwenyekiti wa zamani wa kamati ya mashindano, Evarist Hagila.

Chapisha Maoni

 
Top