FT: Everton 2-1 Gor Mahia
Dakika ya 90: Mwamuzi wa akiba anaonyesha dakika 6 za nyongeza
Dakika ya 87: Gor Mahia wanarudi nyuma kuzuia.
Dakika ya 82: Everton wanapata bao la pili kupitia kwa Kieran Dowell ambaye anawatoka walinzi wa Gor Mahia na kupiga shutli ambalo limejaa wavuni moja kwa moja.
Dakika ya 76: Everton wanapata kona, inapigwa ndegu na kupigwa kichwa lakini inatoka nje inakuwa goal kick.
Dakika ya 70: Kasi ya mchezo imeongezeka upande wa Everton, wanafanya mshambulizi mara kadhaa.
Dakika ya 65: Everton wanafanya shambulizi kali lakini wanakosa umakini mpira unatoka nje.
Dakika ya 55: Kumbuka matokeo bado ni 1-1, Kocha wa Everton, Dylan Kerr anatoa maelekezo mara kadhaa kwa wachezaji wake.
Dakika ya 53: Kasi inaendelea na sasa Everton wanaonekana kujipanga zaidi kwa kutengeneza nafasi kadhaa.
Dakika ya 49: Kasi ya mchezo inaendelea lakini siyo kubwa kama ilivyokuwa kipinsi cha kwanza.
Kipindi cha pili kimeanza.
MAPUMZIKO
Dakika ya 52: Timu zote zinaendelea kushambuliana kwa zamu
HT: Mapumziko bado Everton 1-1 Gor Mahia
45; Bado dakika moja timu ziende mapumziko, huku wakiendelea kushambuliana kwa kasi
Dakika ya 39: Timu zote zinaendelea kushambuliana kwa zamu, mabao bado moja moja
Dakika ya 38: Goooooooooooooooo Gor Mahia wanasawazisha bao
Dakika ya 34 Goooooooooooooooooooooooo Rooney anafunga bao la kwanza
Dakika ya 30, Everton wanaongoza kwa kumiliki mpira huku Rooney akiendelea kudhibitiwa vikali.
Dakika ya 27 bado Rooney hajaonesha makali yake kama alivyodhaniwa na wengi timu ya Gor Mahia wanaonekana kuwadhibiti Everton.
Dakika ya 16 bado timu zote zinashambuliana kwa zamu,
Dakika ya 12 bado Everton 0-0 Gor Mahia.
Chapisha Maoni