0
Wakongomani wanaoishi Tanzania, leo wametoa mpya baada ya kuingia Uwanja wa Ndege wa Julius Nyerere wakiwa na vingoma wakiimba nyimbo mbalimbali kwa kile walichosema kumlaki mchezaji wao anayecheza nafasi ya wingi, Yannick Bolasie.
Mashabiki hao walifika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, JNIA wakiwa na basi aina ya Coaster mbili zikiwa zimefunga bendera kubwa ya DR Congo huku wakiimba na kucheza.
Walianza kucheza kwenye lango kuu la kutokea VIP kabla ya kuhamia kwenye kizuizi cha kutokea uwanjani hapo na kuanza kucheza huku wakipiga ngoma na kuimba.
Mmoja wa mashabiki hao aliyejitambulisha kwa jina la Francesca Bazuku alisema kuwa wameamua kumshangilia Bolasie kwa kuwa wanampenda kutokana na soka yake.
“Sisi ni bapenzi ba Ligi Kuu na tunaipendaga Everton kwa kuwa iko na mchezaji wetu anacheza huko, tunampenda Bolasie na Ligi Kuu ya England na hii tunampa heshima kubwa ajue tunamheshimia,” alisema kwa Kiswahili cha Kikongo.

Chapisha Maoni

 
Top