0
Mshambuliaji wa zamani wa Manchester United, Wayne Rooney ameonekana kama mtu ‘special’ baada ya kulakiwa na kusindikizwa na watu watatu hadi kwenye gari.
Tofuati na wachezaji wengine, kila mmoja alitoka kivyake VIP Lounge na kuelekezwa kumsabahi Waziri Mwakyembe na kuingia ndani.
Wa kwanza kutoka kwenye VIP ni kocha David Koeman ambaye alikwenda moja kwa moja kukaa nyuma ya basi, na kufuatiwa na wachezaji wengine.
Kati ya wachezaji hao, Rooney alionekana kama mtu maalumu, kwani hakutoka peke yake, kulikuwa na watu kama watatu wakimsindikiza na kumpeleka moja kwa moja kwa Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk Harrison Mwakyembe na baada ya kusalimiana alisindikizwa kwenye basi na waliokuwa wakimsindikiza kuishia mlangoni.
Baada ya kufika mlango wa basi, alionyeshwa wapi pa kuweka mzigo wake, kwenye buti na kisha kuingia ndani na wale wasindikizaji kurudi ndani.

Chapisha Maoni

 
Top