Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) limetangaza ratiba ya Ligi Kuu Bara msimu wa 2017-18, huku mechi ya watani wa jadi
Simba na Yanga ikipangwa Oktoba 14 siku ya kumbukumbu ya kifo cha Baba wa Taifa, Julius Nyerere.
Kwa mujibu wa ratiba hiyo mzunguko wa kwanza wa Ligi Kuu Tanzania Bara utaanza Agosti 26, baada ya mechi ya Ngao ya Jamii itakayochezwa Agosti 23, pia itawakutania Yanga bingwa na Ligi Kuu dhidi ya Simba bingwa wa Kombe la FA kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Mchezo wa Oktoba 14 utachezwa siku ya kumbukumbu ya kifo cha Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere itachezwa kwenye Uwanja wa Taifa.
Wakizungumzia michezo hiyo ya Oktoba 14, viongozi wa Simba na Yanga wameonekana kuvutiwa na ratiba huku kila upande ukisema lake kuelekea michezo hiyo.
Katibu wa Yanga, Charles Boniface Mkwasa amesema wamepokea ratiba na kikubwa wataifanyia kazi na ubora wa kikosi chao utaonekana siku husika.
Meneja wa Simba, Musa Hassan Mgosi amesema wao hawana presha kuelekea michezo hiyo na kikubwa wanachoendelea nacho ni maandalizi.
Simba itafungua msimu kwa kucheza na Ruvu Shooting Jumamosi ya Agosti 26, wakati mabingwa Yanga watakuwa wenyeji wa Lipuli Jumapili Agosti 27.
Michezo mingine ya ufunguzi itakayocheza Jumamosi ya Agosti 26, itawakutanisha Ndanda watakuwa wenyeji wa Azam, wakati Mwadui itawakaribisha mataji wapya Singida United, huku Mtibwa itaonyeshana kazi na Stand United.
Kagera Sugar watakuwa wenyeji wa Mbao, wakati Njombe Mji watakuwa nyumbani kuivaa Prisons nayo Mbeya City itaonyeshana kazi na Majimaji kwenye Uwanja wa Sokoine, Mbeya.
Ratiba ya ufubguzi
Jumamosi 26/08/2017
Ndanda v Azam
Mwadui v Singida
Mtibwa v Stand
Simba v Ruvu
Kagera v Mbao
Njombe v Prisons
Mbeya v Majimaji
Jumapili, 27/08/2017
Yanga v Lipuli
Chapisha Maoni