0
Waziri wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo, Dk Harrison Mwakyembe amesema amefarijika na neema kwa ujio wa wachezaji na viongozi wa Everton waliowasili leo.
Wachezaji na viongozi wa timu hiyo waliwasili leo saa 2:15 asubuhi na kulakiwa na Waziri Mwakyembe.
Dk Mwakyembe alisema kuwa ujio wa timu hiyo utaibeba Tanzania, kuitangaza kimataifa kwa kuwa vyombo mbalimbali vya habari vitakuwa vikiiangaza Tanzania.
“Siku zote watakazokuwa nchini, wataifanya Tanzania itangazike, isikike kwani tayari hata SuperSport wamefunga mitambo yao hapa,” alisema Dk Mwakyembe akiwa Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere leo.
Kwenye Uwanja wa Ndege wa Julius Nyerere, mashabiki walifika kuwaona kikiwemo kikundi cha Wacongoman waliokuja kumlaki mchezaji wao anayechezea timu hiyo, Yannick Bolasie.
Msafara wa Everton ambao ni mara ya kwanza kufika nchini, ulikuwa na wachezaji 80.

Chapisha Maoni

 
Top