Kocha wa Chelsea, Antonio Conte ametenga Pauni 50 milioni kudaka saini za nyota wawili, Ross Barkley na Alex Oxlade-Chamberlain ili kuimarisha zaidi kikosi chake.
Chelsea mpaka sasa inawachezaji wa kigeni 17 katika kikosi cha wachezaji 25 na hivi sasa kocha huyo amemgeukia pia kiungo wa Everton, Barkley.
Pia Oxlade-Chamberrlain (23) ambaye anaingia mwaka wa mwisho wa mkataba wake kabla ya kumalizika Arsenal, amekuwa kwenye rada za Conte msimu huu.
Chelsea ipo tayari kufanya mazungumzo ya Everton ili kuvunja mkataba wa Barkley ambao umebaki mwaka mmoja kumalizika.
Hata hivyo habari kutoka Everton, zinaeleza kwamba mchezaji huyo amegoma kuongeza mkataba kwenye klabu hiyo.
Kocha Wa Everton, Ronald Koeman aliweka bayana kwa klabu inayomhitaji mchezaji huyo itapaswa kuweka mezani dau la Pauni 25 milioni.
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni (Atom)
Chapisha Maoni