Ndanda imeanza kusuka kikosi chake kwa kumsajili kiungo Jabir Aziz 'Stima' kwa mkataba wa mwaka mmoja huku wakiwa mbioni kumalizana na mshambuliaji Malimi Busungu kutoka Yanga.
Usajili wa Aziz kutokea Ruvu Shooting ni moja ya jitihada za uongozi wa Ndanda unaosaka kuijenga timu yake baada ya kuondokewa na wachezaji nane wa kikosi cha kwanza.
Mbali ya mkongwe Stima wengine waotegemewa kusajili wakati wowote kutoka sasa ni mshambuliaji Busungu, Ibrahim Job wa Stand United na Hamad Wazir wa African Lyon wako tayari Mtwara kukamilisha mazungumzo yao.
Pia, timu hiyo imemuongezea mkataba kipa wake wa Jeremia Kisubi pamoja na beki Abuu Ubwa.
Wachezaji wa Ndanda walitimka ni mshambuliaji Riffat Hamis aliyejiunga na Mtibwa Sugar wakati kiungo Nassor Kapama yuko mbioni kutua Majimaji ya Songea.
Ndanda imeanza mazoezi kwenye Uwanja wake wa nyumbani wa Nangwanda Sijaona Mtwara ikiwa chini ya kocha mpya Malale Hamsini anayechukua nafasi ya Meja mstaafu Abdul Mingange.
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni (Atom)
Chapisha Maoni