0
KIUNGO mshambuliaji wa Simba, Mohamed Ibrahim, amekubali kuwa juzi Alhamisi ilikuwa ni siku ya staa wa Everton, Wayne Rooney, na hakuna kitu kingine ambacho ungeweza kuwaambia Watanzania wakaelewa.
Rooney aliiongoza Everton kuifunga Gor Mahia mabao 2-1 Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam, huku akitangulia kufunga bao kabla ya Kieran Dowell kufunga la ushindi.
“Imeleta mwamko wa kujituma na kujua jinsi ambavyo wadau wanapenda soka, kwani haikuwa hali ya kawaida kila kona alikuwa anatamkwa Rooney kana kwamba hakukuwepo na wachezaji wengine,” alisema.
Nyota huyo alisema kwa sasa anaziweka kando stori za Rooney na badala yake anaelekeza akili yake kujifua kwa ajili ya mechi ya Ngao ya Jamii.
“Mbele yetu kuna kazi kubwa ambayo Watanzania, wanaisubiri licha ya kwamba kila mtu anaongelea Rooney, ikumbukwe kwamba Agosti 23, itakuwa zamu yetu ambapo mashabiki watataka kujua kwamba tuna jipya gani,” alisema.

Chapisha Maoni

 
Top