Mshambuliaji mpya wa Everton, Wayne Rooney amethibitisha kwamba atakuja Tanzania wiki hii kucheza mechi ya kirafiki ikiwa ni maandalizi ya msimu ujao wa Ligi Kuu England.
Rooney amesema safari hiyo y maandalizi ya Everton nchini Tanzania ni nafasi nzuri kwake kuwajua wachezaji wenzake.
Mshambuliaji huyo kinara wa ufungaji wa wakati wote wa timu ya taifa ya England amejiunga na klabu yake ya utotoni Blues juzi Jumapili kwa kusaini mkataba wa miaka mwili ndani ya Goodison Park.
Rooney alifika kwa mara ya kwanza leo kwenye uwanja wa mazoezi wa USM Finch Farm atakuwa moja wa wachezaji wa timu hiyo itakayokwenda Afrika Mashariki wiki hii chini ya kocha Ronald Koeman kwa ajili ya mchezo moja wa kirafiki dhidi ya mshindi wa SportPesa Super Cup, Gor Mahia, utakaofanyika Alhamisi.
Safari hiyo ni kusherekea kufanikishwa kwa rekodi hiyo ya mkataba baina ya klabu ya Everton pamoja na kampuni ya michezo ya kubahatisha ya SportPesa.
Mshambuliaji huyo miaka 31, tayari anajuana na wachezaji baadhi waliopo katika kikosi cha sasa cha Everton akiwamo Morgan Schneiderlin, Michael Keane aliokuwa nao Manchester United, wengine ni Phil Jagielka, Leighton Baines na Ross Barkley aliocheza nao katika timu ya taifa.
Sasa Rooney anajianda kuwajua vizuri wachezaji wenzake wa kikosi hicho wakati wa ziara ya Tanzania.
“Nipo tayari kwa hilo, najua itakuwa safari nzuri,” aliimbia evertontv. “Itakuwa ni vizuri na matumaini yangu nitapata nafasi ya kucheza mechi uwanjani pia.
“Inakuwa ni vizuri unapokuwa safarini na timu. Yanakuwa mazingira mazuri nampokuwa hoteli na wachezaji wengine na kupata muda wa kuwa pamoja na kujuana zaidi.
“Sijawahi kufika Tanzania, kwa hiyo nategemea kuona mambo mazuri ya huko.”
Chapisha Maoni