0

Mgombea wa nafasi ya Ujumbe wa kamati Tendaji ya Shirikisho la Soka nchini TFF Kanda ya Dar es Salaam, Shaffih Dauda ametangaza kujiengua katika nafasi hiyo kwa kile alichokitaja kuwa ni kulinda Jina lake baada ya kuhusishwa na tuhuma za Rushwa.
Dauda ambaye Jumanne alikamatwa na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na mkoa wa Mwanza Kwa tuhuma za kufanya Kampeni Mapema Kabla ya Wakati, Kampeni ambazo zilihusishwa na Rushwa ametangaza kujiuzulu Leo asubuhi kupitia Kipindi cha 360 Cha Clouds TV.
-Unapofanya jambo lazima uangalie mwisho wake kuna manufaa gani? Nimeamua kwa maslahi mapana ya mchezo wa soka na kulinda heshima ya jina langu kwa nia njema nimeamua kujiuzulu kugombea nafasi ya ujumbe kamati ya utendaji TFF." Amesema.
Aliendelea kusema "Nitaendelea kushirikiana na Viongozi wa Soka kama hapo awali, kushauri na kutoa maoni yangu kama mdau katika kukuza na kuendeleza mpira wa miguu Tanzania".
Pamoja na Hayo Shaffih Alisema kuwa "Kuonyesha uwajibikaji ni jambo Jema! Nipo kwenye mfumo wa Mpira muda mrefu naijua mizengwe na fitna kuna watu nyuma yangu wanaonitizama ukichafuliwa kwa Rushwa ni kuharibu future yako" Alisema.
Waliokamatwa.
Ikumbukwe kwamba Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa 'TAKUKURU' Mkoa wa Mwanza ilothibitisha kuwashikilia na kuwaachia Kwa Dhamana wagombea wanne wa nafasi ya Ujumbe katika uchaguzi mkuu wa Shirikisho la Soka nchini TFF.
Mbali na Hao ambao ni wagombea TAKUKURU pia imethibitisha kuwakamata Wajumbe 10 ambao ni Wapiga kura katika uchaguzi huo ambao utafanyika Agosti 12 Mwaka huu Mjini Dodoma.
Wagombea ambao walikamatwa na kuachiwa kwa Dhamana ni pamoja na Shaffih Dauda, Elias Mwanjali, Benista Lugola na Ephraim Majinge.


Chapisha Maoni

 
Top