Timu ya soka ya African Lyon imefanikiwa kurejea tena katika mikimiki ya ligi kuu soka Tanzania Bara baada ya kuibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Kiluvya United katika mchezo wa mwisho wa kundi A.
African Lyon wanaungana na JKT Tanzania katika kundi A kucheza ligi kuu msimu wa 2018/19.
Katika mchezo huo ambao umefanyika katika uwanja wa Filbert Bayi uliopo Kibaha mkoani Pwani, African Lyon wamepata bao pekee katika kipindi cha kwanza kupitia kwa Kassim Mdoe.
Kuhitimishwa kwa ligi daraja la kwanza kunatoa fursa kwa timu Sita kucheza ligi kuu msimu ujao ambazo ni JKT Tanzania, African Lyon na Kinondoni Municipal Council kutoka Jijini Dar es Salaam.
Nyingine zilizopanda daraja ni Alliance School ya Mwanza, Coastal Union ya Tanga na Biashara United kutoka mkoani Mara.
Chapisha Maoni