0
Timu ya soka ya Simba imefanikiwa kufuzu hatua ya kwanza ya michuano ya kombe la Shirikisho Afrika baada ya kuwatoa Gendarmerie Tnale ya Djibouti Kwa jumla ya mabao 5-0
Simba wamefikisha idadi hiyo ya mabao baada ya kuibuka na ushindi wa bao 1-0 Katika mchezo wa duru ya pili uliofanyika kwenye uwanja wa Stade du Ville nchini Djibouti.
Katika mchezo huo, timu zilikwenda mapumziko bila ya kufungana, Nani ndipo katika kipindi cha Simba waliandika bao la kuongoza na la pekee katika mchezo huo kupitia kwa mchezaji wa kimataifa wa Uganda Emmanuel Okwi.
Ikumbukwe katika mchezo wa duru ya kwanza uliopigwa jijini Dar es Salaam Simba waliibuka na ushindi mnono wa mabao 4-0 mabao ambayo yalifungwa na John Bocco, Said Ndemla na Emmanuel Okwi.
Sasa Simba watakutana na El Masry ya Misri katika hatua inayofuata baada ya wao kuwatoa Green Buffalos ya Zambia kwa jumla ya mabao 5-2 baada ya mchezo wa duru ya pili kumalizika kwa Buffalos kuibuka na ushindi wa mabao 2-1, mchezo ukifanyika nchini Zambia.
Kikosi cha Simba kilichocheza.
Kilichoanza: Aishi Manula, Nicholas Gyan, Juuko Murushid,.Asante Kwasi, Yusuph Mlipili, Erasto Nyoni, Jonas Mkude, James Kotei, Mzamiru Yassin, Emmanuel Okwi na Shiza Kichuya.
Benchi: Emmanuel Mseja, Mohamed Hussein, Mwinyi Kazimoto, Moses Kitandu, Paul Bukaba, Ally Shomari na Said Hamis Ndemla.

Chapisha Maoni

 
Top