0
 Mbao FC, kimeibuka na ushindi kwenye Uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza, baada ya kuitandika
Kagera Sugar mabao 2-1, katika mchezo ligi kuu.
Mbao walipata bao la kuongoza dakika ya 61, likipachikwa na James Msuva kwa shuti kali.
Kikosi hicho kinachomilikiwa na wafanyabiashara wa mbao Mwanza, walipachika bao la pili dakika ya 70, lililofungwa na Habib
Kiyombo, hata hivyo, dakika nne baadaye, Kagera walipata bao pekee la kufutia machozi likifungwa na Atupile Green.
Ushindi huo, umeifanya Mbao kufikisha pointi 18, huku Kagera ikiendelea kubaki na alama 13.

Chapisha Maoni

 
Top