0
KIKOSI cha Alliance FC cha jijini Mwanza, leo Jumapili kimeweka historia mpya kwenye medani za soka baada ya kufudhu kucheza Ligi Kuu Bara msimu ujao kwa kuilaza JKT Oljoro mabao 2-1.
Mchezo huo uliokuwa wa mwisho kwenye Ligi Daraja la kwanza kwa kundi C, umepigwa kwenye Uwanja wa Nyamagana, Mwanza na kuhudhuriwa na maelfu ya wadau wa soka ambao
walishuhudia Alliance wakikata tiketi hiyo rasmi.
Mabao mawili yaliyofungwa na Dickson Ambundo dakika ya 13, kwa njia ya mkwaju wa
penalti na Athanas Mdamula dakika 47, yalitosha kuwazima Maafande wa Oljoro walioambulia bao moja lililopachikwa a Kuha Fabian dakika ya 82.
Ilikuwa ni furaha,shangwe na vifijo kwa mashabiki wa Alliance na wadau wa soka
jijini Mwanza baada ya kushuhudia timu yao kutarajia kuzileta Simba na Yanga mkoani
Mwanza msimu ujao.
Ushindi huo wa leo,umeiweka Alliance nafasi ya pili kwa pointi 28 wakitanguliwa na Biashara pointi 30, katika kundi lao C lililokuwa na timu nane za Dodoma,Rhino,Oljoro,Trans Camp,Pamba na Toto Africans.

Chapisha Maoni

 
Top