0
Arsenal imepata ushindi wake wa kwanza msimu huu baada ya kuichapa West Ham kwa mabao 3-1, huku Everton ikilazimishwa sare 2-2 AFC Bournemouth katika mechi iliyoshudia kadi nyekundu mbili.

Katika mchezo huo mabao ya Arsenal yalifungwa na Nacho Monreal, bao la kujifunga Issa Diop pamoja na Danny Welbeck wakati lile la kufutia machozi kwa West Ham lilifungwa na Arnautovic
Huo ni ushindi wa kwanza kwa kocha Unai Emery tangu alipochukua jukumu la kuinoa Arsenal, wakati West Ham ikipata kipigo cha tatu mfululizo.

Everton ilishindwa kulinda ushindi wake wa mabao 2-0 baada ya kukubalia Bournemouth wasawazishe katika mchezo ulioshudia timu zote zikimaliza zikiwa na wachezaji 10 kutokana na kadi nyekundu.

Nyota wa Everton, Richarlison alitolewa nje kwa kadi nyekundu dakika 41, kabla ya kuongoza kwa mabao 2-0 yaliyofungwa na Theo Walcott na Michael Keane.
Bournemouth ambao Adam Smith alitolewa nje wakiwa nyuma kwa bao 1-0, lakini walifanikiwa kusawazisha kwa mabao ya Joshua King aliyefunga kwa penalty na Nathan Ake.

Southampton ilikuwa ya kwanza kupata bao la kuongoza dhidi ya Leicester City kupitia Ryan Bertrand, lakini Demarai Gray alisawazisha kwa wageni kabla ya Pierre-Emile Hojbjerg kutolewa nje kwa kadi ya pili ya njano.
Katika dakika ya 91, Harry Maguire aliifungia Leicester City bao la ushindi 2-1.

Katika mchezo mwingine Huddersfield ilipata pigo baada ya mchezaji wake Jonathan Hogg kupewa kadi nyekundu ya moja kwa moja wakati timu yake ikilazimishwa suluhu na Cardiff.
Matokeo

Wolverhampton Wanderers 1 - 1 Manchester City

 AFC Bournemouth 2 - 2 Everton

Arsenal 3 - 1 West Ham United

Huddersfield Town 0 - 0 Cardiff City

Southampton 1 - 2 Leicester City

Chapisha Maoni

 
Top