0
. Mshambuliaji Meddie Kagere ameendelea kuthibisha ubora wake baada ya kufunga mabao mawili Simba ikichapa Mbeya City 2-0 kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Mabao hayo mawili ya Kagere yanamfanya kuongoza katika orodha ya wafungaji wa Ligi Kuu baada ya kufikisha magoli matatu katika mechi mbili alizocheza hadi sasa.
Kagere alianza kuipatia Simba pointi tatu katika mchezo wa kwanza wa ligi dhidi ya Tanzania Prisons baada ya kufunga bao 1-0 na leo ameonyesha kuendelea kuonyesha msaada zaidi kwa timu yake baada ya kupachika bao mbili kwa kichwa dakika ya 12 na 45 yote akikwamisha kwa kichwa.

Simba iliyoingia katika mchezo huo kwa kasi na kutumia mipira ya juu ilifanikiwa kupata bao la kuongoza dakika 12, kwa Kagere kuunganisha kwa kichwa krosi ya Shiza Kichuya.
Baada ya bao hilo Mbeya City ilibadilika na kuongeza umakini katika ulinzi na kuwazuia Simba wasipitishe mipira ya krosi kwa washambuliaji wao Kagere na John Bocco.
Katika mchezo huo Mbeya City ilifanikiwa kumtuliza kiungo wa Simba, Hassan Dilunga asicheza kwa huru jambo lililopooza mashambulizi ya mabingwa hao.
Kagere alifunga bao la pili katika dakika 45, akiunganisha krosi ya Asante Kwasi.
Dakika ya 15 Mbeya City walifanya shambulizi lililozaa kona ambayo haikuwa na madhara langoni mwa Simba baada ya Majaliwa Shabani shuti lake kupaa juu ya lango.

Dakika ya 36 Kapombe alipiga krosi safi ndani ya boksi iliyomkuta Bocco ambaye alishindwa kutumia nafasi ya wazi na kutoa pasi kwa Kwasi ambaye alichelewa na mpira kuokolewa na mabeki wa Mbeya City.
Hadi mapumziko Simba iliondoka kifua mbele kwa kufunga bao 2-1 bao la pili limefungwa na Meddie kagere aliyeunganisha mpira kwa kichwa baada ya krosi safi iliyochongwa na Kwasi.

Kipindi cha pili kimeasha kwa timu zote kushambuliana kwa zamu lakini safu ya ushambuliaji ya kila timu ipo makini dakika ya 51 simba imefanya mabadiliko kwa kumtoa Aishi Manura na nafasi yake kuchukuliwa na Ally Salim.
Dakika 59 simba wameshindwa kutumia nafasi ya wazi baada ya mabeki wa mbeya wakimuacha Kichuya apige krosi kwa kuzani kwamba ameotea lakini Bocco alishindwa kukwamisha mpira nyavuni kutokana na shuti lake kuokolewa na kipa Owen Chaima.
Mbeya City pamoja na kuonyesha jitihada za kucheza vizuri kipindi cha kwanza hawajapiga shuti hata moja la hatari langoni mwa Simba.

BOCCO AANZA NA GUNDU
Mshambuliaji wa Simba Jonh Bocco ambaye amepata nafasi ya kuanza mechi zote mbili ameshindwa kuonyesha makali yake ya kufumania nyavu katika michezo yote aliyocheza.

Bocco alianza katika mchezo wa ngao ya jamii dhidi ya Mtibwa hakuwesa kupachia bao, dhidi ya Prisons pia na katika mchezo dhidi ya Mbeya City ameshindwa kufanya ivyo na kufanyiwa sabu dakika ya 83 nafasi yake ilichukuliwa na Adam Salamba ambaye ni kama hakuwa na msaada kwa timu kutokana na kushindwa kupiga shuti hata moja langoni kwa wapinzani wake.
Hadi dakila tisini zinaisha simba wameibuka na usjindi wa bao 2-0 na kufanikiwa kufikisha pointi sita ambazo zitategemea na michezo mingine ya ligi inayochezwa ili aweze kuongoza ligi.

Mazoezi krosi
Simba katika mchezo huo waliingia na mbinu ya kutumia mipira ya juu na kupiga krosi jambo lililowasaidia kupata bao la mapema.

Katika mazoezi yao kabla ya kuanza kwa mechi Simba ililifanya kwa ajili ya kupasha moto misuli kabla ya mchezo huo ni lililenga zaidi mipira ya krosi hiyo ingawa walifanya pia ya kucheza mpira.
Washambuliaji pamoja na viungo ndiyo walilengwa zaidi.
Viungo walianzisha mawinga walipiga krosi na washambuliaji kumalizia.

Winga Shiza Kichuya ndiyo alitumika zaidi katika upigagaji wa mipira ya krosi akitokea upande wa kushoto na washambuliaji wa kati Mnyarwanda Kagere na John Bocco 'Adebayor' walimalizia.

Mabeki walioongozwa na Pascal Wawa pamoja na Erasto Nyoni walikuwa wanacheza kukabana peke yao.
Mazoezi hayo yamesimamiwa na Mtunisia Adel Zrane na Mrundi Masoud Djuma mkuu wao Patrick Aussems aliingia kusimamia mechi.

VIKOSI
Simba: Aishi Manula, Shomari Kapombe, Asante Kwasi, Pascal Wawa, Erasto Nyoni, Jonas Mkude, James Kotei, Hassan Dilunga, Meddie Kagere John Bocco na Shiza Kichuya.

Mbeya City : Owen Chaima, John Kabanda, Mpoki Mwakinyuki, Erick Kialuzi, Ibrahim Ndunguli, Majaliwa Shabani, Mohamed Kapeta, Medson Mwakatundu, Chunga Said, Bakari Masoud na Eliud Ambokile

Chapisha Maoni

 
Top