Makamu Rais wa zamani wa FIFA amehukumiwa kifungo cha miaka tisa gerezani nchini Marekani ikiwa ni matokeo ya uchunguzi wa ruhswa iliyofanywa ndani ya chombo hicho kikubwa cha soka duniani.
Juan Angel Napout, ambaye anatokea Paraguay alipatikana na hatia ya kuchukua mamilioni ya dola kwa njia ya rushwa.
Hatua hii inakuja siku chache baada ya kifungo cha miaka minne alichopewa mkuu wa zamani wa soka Brazil Jose Maria Marin ambaye pia alihusishwa kwenye tuhuma hizohizo.
Wote kwa pamoja walikutwa na hatia ya kupokea rushwa kutoka kwa makampuni makubwa ambayo yalikua yakijitangaza kupitia FIFA.
Chapisha Maoni