0
Kocha mkuu wa Timu ya Tanzania, Taifa Stars, Emmanuel Amunike, amewaondoa wachezaji 6 wa Simba kwa kosa la kuchelewa kuripoti kambini isipokuwa Mlindalango Aishi Manula.
Wachezaji hao isipokuwa Manula aliyewahi kambini, walitakiwa kuripoti siku ya Jumatatu baada ya kumalizika kwa mchezo wa dhidi ya Mbeya City lakini walishindwa kufanya hivyo.
Wachezaji hao ni Nadhodha John Bocco, Shiza kichuya, Jonas Mkude, Erasto Nyoni, Shomari Kapombe pamoja na Hassan Dilunga.
Kwa upande wa viongozi wa Simba ambao ni Meneja wa Klabu, Richard Robert ,pamoja na Kaimu Katibu Mkuu, Hamis Kisiwa, Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini (TFF) kwa kufuata kanuni limewapeleka kwenye Kamati ya Maadili kwa kutotimiza wajibu wao.
Baada ya kuondolewa, wachezaji walioitwa kuchukua nafasi zao ni Paul Ngalema wa Lipuli FC, Salumu Kimenya wa Tanzania Prisons, David Mwantika na Frank Domayo wa Azam FC, Salumu Kihimbwa na Kelvin Sabato wa Mtibwa Sugar na Ali Abdulkadir.

Chapisha Maoni

 
Top