majina yanayofanya vizuri katika muziki
wa Injili barani Afrika hasa kutokana na
uwezo wake jukwaani pindi anapofikisha
uinjilishaji kwa waamini na mashabiki
mbalimbali.
Muhando ni mzaliwa wa kijiji cha
Dumila, wilaya ya Kilosa, Mkoa wa
Morogoro, Tanzania, Afrika Mashariki na
ni mwimbaji wa nyimbo za injili kwa lugha ya Kiswahili ambaye umahiri wake awapo jukwaani umefanikisha kutambulika barani Afrika.
Rose atakayepanda jukwaani kuanzia
Desemba 25, Agosti 3 mwaka huu alizindua albamu yake Kamata Pindo la Yesu yenye nyimbo za ‘Facebook’, ‘Bwana Niongoze’,
‘Wewe Waweza’, ‘Usiniache’, ‘Nibariki na
Mimi’, ‘Usivunjike Moyo’ na ‘Kwema’.
Awali Rose kabla hajawa Mkristo alikuwa
Muislam na ni mama wa watoto watatu.
Alimpokea Yesu Kristo pale alipokuwa
anaumwa na yuko kitandani akiwa na
umri wa miaka 9, aliugua kwa muda wa
miaka mitatu na baadae alipona na
kubadili dini na kuwa Mkristo.
Rose alizama kwenye muziki katika kwaya iliyoko Dodoma na alikuwa mwalimu wa Kwaya katika kwaya ya Dodoma St. Mary’s katika kanisa la Kianglikana la Chimuli.
Januari 31 mwaka 2005, Rose Muhando
alizawadiwa tuzo ya Mtunzi bora wa
nyimbo za Injili, Mwimbaji Bora na albamu Bora ya Mwaka.
Tuzo hizo zilitolewa katika Tamasha Tanzania Gospel Music Awards,
2004.Desemba mwaka 2005 alihudhuria
katika tamasha la Nyimbo za Injili katika
kusaidia kuchangia kwa watoto na wajane Dar es Salaam ambapo alitekeleza ipasavyo uchangiaji huo.
Februari 2011, Rose Muhando alisaini
mkataba na Mult Album Recording Deal na Kampuni ya Sony Music ya Afrika Kusini.
Kusaini huko kulitangazwa katika mkutano wa waandishi wa habari Dar es Salaam, Tanzania na hiyo ni mara ya kwanza kufanyika Afrika Mashariki. Baadhi ya albamu za Rose Muhando ni:
1. Mteule uwe macho, 2004
2. Kitimutimu, 2005
3. Jipange sawasawa, 2008
4.Utamu wa Yesu 2012
4.Kamata Pindo la Yesu 2014
Tuzo alizopata
2005 -Tanzania Music Awards: Mwimbaji
Bora wa Kike Nyimbo za Dini (“Mteule uwe
macho”)
2009 - Mwimbaji Bora wa Nyimbo za Injili
2008- Alitunukiwa tuzo nchini Kenya ya
Mwimbaji Bora wa Injili Afrika
Amewahi kuzawadiwa kitita cha
Sh200,000 na Shirika la Utangazaji la Taifa (TBC).
Chapisha Maoni