Neno “piga” lina maana ya “fanya kitendo cha kukutanisha vitu kwa nguvu, fumua, ezeka, zaba, shambulia, chapa na tandika” kwa mujibu wa Kamusi ya Kiswahili Sanifu, Oxford, lakini kwa
Waziri Mkuu Mizengo Pinda neno “wapigeni” lilimaanisha “kuendelea kulinda amani”. ‘‘Baada ya kutoa kauli hiyo kuna watu wakaeleza kuwa sasa Waziri Mkuu analeta sera za kupiga.
Hapana ilikuwa kujaribu kukemea watu wasilete fujo kama kwamba Serikali iko likizo,’’ alisema Pinda.
Alisema akiwa bungeni aliwahimiza Watanzania kuilinda amani na utulivu uliopo nchini kwa gharama yeyote ile na iwapo atatokea mtu kutaka kuivunja amani hiyo, hatapewa nafasi badala yake atashughukiwa kwa namna yeyote.
Waziri Pinda alitoa kauli hiyo tata mwaka jana wakati wa kipindi alichokianzisha bungeni cha mswali ya papo kwa papo kwa Waziri Mkuu,
baada ya kluulizwa kuhusu vitendo vya polisi kupiga rais badala ya kuwafikisha mahakamani.
Kauli yake ilisababisha wanaharakati kumjia juu na wengine kutaka kwenda mahakamani kutokana na kwenda kinyume na misingi ya utawala bora.
Waziri Pinda alitoa tafsiri ya neno hilo alipoongea na wananchi wa Mkoa wa Katavi wakati akihitimisha ziara yake kwa kukutana na wananchi wa Tarafa ya Kabungu, Kata ya Mpanda Ndogo
wilayani Mpanda.
Alisema amani iliyopo hapa nchini ni ya miaka mingi iwapo wakitokea watu wanaotaka kuleta chokochoko, watashughulikiwa tu.
Akizungumzia wakimbizi walioko mkoani Katavi ambao wanatarajiwa kupewa uraia, alisema ni lazima mkoa ujiandae kuwapokea raia hao wapya
na hiyo nayo ni changamoto kubwa kwa mkoa. ‘‘Wakimbizi hao wanaotarajiwa kupewa uraia ni wengi kwani ni zaidi ya 120 na changamoto kubwa iliyo mbele ya mkoa.
Hivyo ni vyema
utaratibu mzuri ukaandaliwa kwa ajili ya
kuwapokea raia hao wapya na mkoa umejiandaa vizuri utalifanyia kazi suala hilo kuhakikisha amani
iliyopo inatunzwa,” alisema.
Alisema mbali ya wakimbizi hao walioko makazi ya Mishamo wapo wakimbizi wengine walioko kwenye makazi ya Katumba ambao nao wanakaribia kufikia 80,000 ambao pia watapewa
uraia.
Chapisha Maoni