HAKI SAWA: Mwenyekiti wa CUF, Profesa Ibrahim Lipumba (kulia) na Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali, Zitto Kabwe wakiwasili kwenye Uwanja wa Mashujaa mjini Mtwara jana, ambako walihutubia mkutano wa hadhara.
Picha na Ibrahimu Yamola Mtwara. Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC), Zitto Kabwe amesema atamuunga mkono Kiongozi wa Kambi Rasmi ya Upinzani, Freeman
Mbowe pale atakapowasilisha hoja yake
bungeni kuhusu ufisadi wa zaidi ya Sh1
trilioni katika mradi wa bomba la gesi
kutoka Mtwara kwenda Dar es Salaam.
Zitto aliyasema hayo jana katika mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye Uwanja wa Mashujaa mkoani hapa uliandaliwa na Chama cha Wananchi (CUF)
kuwashukuru wakazi wa mkoa huo kwa
kuwachagua viongozi wa chama hicho
katika uchaguzi wa Serikali za Mitaa.
“Najua bado mnalia kuhusu bomba la
kupeleka gesi Dar es Salaam, machozi
yenu yatafutika kwani tayari habari za
ufisadi mkubwa katika ujenzi wa bomba
hili zimeanza kuchomoza.
“Kiongozi wa Upinzani Bungeni (Mbowe)
ametamka mara kadhaa kuwa atatoa
hoja kuhusu ufisadi katika ujenzi wa
bomba la gesi. Pale atakapohitaji msaada
wetu tutamsaidia, tunaamini gharama za
mradi huu zimezidishwa mara mbili na
inawezekana kabisa kuwa zaidi ya Dola
ya Marekani 600 milioni (zaidi ya Sh1
trilioni) zimegawanywa kwa watu kama
rushwa kuanzia China mpaka hapa
Tanzania. Machozi yenu wana Mtwara
yatafutwa kwa uwezo wa Mola,” alisema
Zitto.
Alisema katika miaka ya hivi karibuni
Mkoa wa Mtwara umechukua sura mpya
kitaifa baada ya kugunduliwa kwa gesi na wao (wananchi) wameonyesha kwamba wakiamua wanaweza kupigania masilahi ya Taifa.
“Mmesimama kidete kuhakikisha utajiri
huu hauporwi na haturudii makosa
yaliyofanyika Kanda ya Ziwa pale
tuliporuhusu madini kuporwa na
mabeberu wa kimagharibi,” alisema.
Mwenyekiti wa CUF, Profesa Ibrahim
Lipumba akiwahutubia wakazi hao,
aliwataka viongozi wa Serikali za Mitaa
waliochaguliwa kuongoza kwa misingi ya chama ya haki sawa kwa wote.
“Profesa Muhongo (Waziri wa Nishati na
Madini, Sospeter) hana uwezo wa
kuendelea kuwapo madarakani na
hapaswi kufumbiwa macho, wote
waliohusika na sakata hili lazima
wachukuliwe hatua,” alisema.
Kuhusu uandikishaji wa Daftari la
Kudumu la Wapigakura alisema,
“watakapokuja kuwaandikisha jitokezeni
hiyo ndiyo njia pekee ya kutafuta
ukombozi wa pili wa Taifa hili lakini
msipofanya hivyo hatutawaondoa hawa
CCM.”
Mapokezi yalivyokuwa
Pilika pilika za mapokezi ya viongozi hao
zilianza tangu asubuhi na ilipofika saa
5.20 zaidi ya magari 40 yaliyopambwa
kwa bendera za CUF, pikipiki 300 na
bajaji 30 zilikusanyika katika daraja la
Mikindani kuwapokea viongozi hao.
Wakiwa wamevalia sare za chama chao,
wafuasi hao walikuwa wakiimba nyimbo
mbalimbali ukiwamo wa “Tunataka
fedha zetu za escrow zirudi... mtumbwi
wa Chenge umetoboka.’
ACT wapata kipigo
Wanachama wa chama kipya cha ACT-
Tanzania waliosafiri kutoka Dar es
Salaam kwenda Mtwara wakitumia basi
dogo aina ya Coaster walikumbana na
kipigo kutoka kwa wafuasi wa CUF
waliowazuia wakidai kuwa
hawakualikwa.
Mmoja wa wanachama wa ACT ambaye
pia ni Mwenyeji wa Mkoa Kigoma
anayeishi Dar es Salaam, Monalisa Ndala alisema; “Tuliambiwa huu mkutano siyo wa kwetu na ACT hawahusiki, ndipo walianza kutupiga wakitutaka kuvua sare kama tunataka kuendelea na msafara.”
Africa Newss
Mwananchi
Chapisha Maoni