0
Jeshi la polisi nchini limetoa ufafanuzi kuhusu
tamko la kupiga marufuku maandamano na
mikutano ya hadhara ya vyama vya kisiasa kuwa
tamko hilo lililenga kuzuia maandamano na
mikutano ya hadhara ya vyama vya siasa na wala
tamko hilo halikupiga marufuku mikutano ya
kiutendaji na kiutawala ya vyama vya siasa
inayofanywa kwa mujibu wa katiba na kanuni za
vyama husika.
Hivyo jeshi la polisi linawataka watu wasipotoshe
watu kuhusu tamko hilo na pale hali ya kiusalama
itakapotengemaa, mikutano na maandamano ya
vyama vya siasa itaruhusiwa kufanyika.
June pili, 2016 Jeshi la polisi nchini lilitoa tamko
lililolenga kuzuia mikutano, maandamano ya
kisiasa nchini kutokana hali za kiusalama.


MillardAyo.com

Chapisha Maoni

 
Top