Dkt John Pombe Magufuli amekumbushwa kupitia
upya mikataba ya kimataifa na kikanda inayotaka
kuwepo na misingi ya usawa wa kijinsia kwenye
ngazi mbalimbali za uongozi.
Wito huo mekuja mara baada ya Mashirika
yanayotetea haki za wanawake na usawa wa
kijinsia nchini kulalamikia uteuzi ambao rais
Magufuli amekuwa akiufanya katika ngazi
mbalimbali za kimaamuzi nchini, kuwa nafasi hizo
haziwapi wanawake fursa kulingana na mikataba
ya kimataifa ambayo Tanzania iliridhia.
Akiongea na waandishi wa habari hii leo jijini Dar
es salaaam kwa niaba ya mashirika mengine,
Mkurugenzi wa mtandao wa jinsia nchini TGNP Bi.
Lilian Liundi Ametaja nafasi hizo kuwa uteuzi wa
baraza la mawaziri, makatibu wakuu, wakuu wa
idara na taasisi, wakuu wa mikoa na wilaya pamoja
na maofisa tawala na wakufugenzi wa almashauri
nchini.
Katika nafasi hizo idadi ya wanawake imepungua
sana kulinganisha na idadi ya wanawake
waliokuwepo katika utawala wa awamu ya nne
ambapo usawa wakijinsia kwa kiasi kikubwa
ulizingatiwa na wanawake kuweza kuwa miongoni
mwa watenda maamuzi katika ngazi mbalimbali za
uongozi.
Bi. Lilian Liundi ameeleza kuwa tangu uteuzi huo
ufanyike kiwango cha idadi ya wanawake kwenye
nafasi za maamuzi imepunguwa kwa kiasi kikubwa
jambo mbalo ameeleza kuwa linarudisha nyuma
juhudi za kuziba pengo lililopo kuelekea usawa wa
50/50.
"Washauri wa rais wamkumbushe juu ya usawa wa
kijinsia, hii inaturudisha nyuma kwa kiwango
kikubwa, kibaya zaidi hata mwanamke akiteuliwa
nafasi ya kuonyesha jinsia haiwekwi na inakuwa
vigumu kutambua nani ni mwanamke nani ni
mwanaume, jambo hili ni muhimu sana kwa ustawi
wa jamii ya wapenda maendeleo" amesema Lilian
Liundi.
EATV
Chapisha Maoni