Mkufunzi wa Liverpool Jurgen Klopp ameweka kandarasi mpya ya miaka sita na mmiliki wa klabu hiyo akisema ingekuwa makosa kutompatia
kandarasi ndefu.
Klopp alijiunga na Liverpool mnamo mwezi Oktoba ,baada ya kukubali mkataba wa pauni milioni 15
ambao umeongezwa hadi mwaka 2022.
''Uongozi wake utakuwa muhimu katika kufanikisha malengo yetu'' ,alisema mmiliki wa Liverpool.
Klopp aliifikisha Liverpool katika fainali ya League Cup pamoja na fainali ya Europa League msimu
uliopita.
Raia huyo wa Ujerumani mwenye umri wa miaka 49 aliisaidia Borussia Dortmund kushinda mataji
mawili ya Bundesliga pamoja na kucheza fainali ya
vilabu bingwa Ulaya 2013.
Chapisha Maoni