Klabu ya As Roma ikicheza ugenini katika dimba la Adriatico imeichapa Pescara, kwa mabao 4-1 na hivyo kuishusha rasmi timu hiyo mpaka Seria B.
Pescara wababuruza mkia katika ligi wakiwa na alama 14 huku wakiwa wamecheza jumla ya michezo 33 msimu huu.
Roma walipata magoli yao kupitia kwa viungo wake Kevin Strootman na Radja Nainggolan, huku
winga mahiri wa timu hiyo Mmisri Mohamed Salah, akitupia mabao mawili.
Kwa ushindi huo Roma wanapunguza wigo wa
alama na vinara wa ligi hiyo Juventus kuwa alama nane baada ya ushindi wa mchezo huu, huku wote wakiwa wamecheza michezo 33.
Wakati huo huo klabbu hiyo ya Roma imemtangaza Ramon Rodriguez 'Monchi' kuwa
mkurugenzi wa michezo wa timu hiyo Monchi alikuwa mkurugenzi wa michezo wa timu ya Sevilla ya Hispania kwa miaka 17 na kuisaidi
timu hiyo kuchukua mataji matatu ya Europa ligi.
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni (Atom)
Chapisha Maoni