Klabu ya Newcastle United msimu ujao watakipiga katika ligi kuu ya England ya baada ya kupanda
tena daraja kutoka Championship kwa kuichapa timu ya Preston kwa mabao 4-1.
Mshambuliaji wa Newcaste Ayoze Perez ndie aliyeanza kuiandika timu yake goli la kuongoza
katika dakika ya saba ya mchezo,Katika dakika ya
kumi na nne Preston wakachomo goli hilo kupitia kwa mshambuliaji wake Jordan Hugill, Kiungo Christian Atsu akaiongezea Newcastle bao
la pili katika dakika ya arobaini na tano ya kipindi cha kwanza, katika dakika ya sitini na tano winga
Matt Ritchie akaongeza bao la tatu kwa vijana wa Rafa Benitez kwa mkwaju wa penati.
Mshambuliaji Ayoze Perez tena akashindilia msumari wa mwisho uliowahakishia Newcastle
kurejea tena katika ligi kuu msimu ujao.
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni (Atom)
Chapisha Maoni