0
Mshike mshike wa kuwania ubingwa ligi kuy ya England utaendelea tena leo kwa mchezo mmoja kupigwa vinara wa ligi hiyo Chelsea watakua katika uwanja wao wa nyumbani kuwaalika watakatifu wa Southampton.
Nahodha wa Chelsea Gary Cahill anatarajiwa kuwa sehemu ya kikosi baada ya kurejea mazoezi baada
ya kupona tatizo la tumbo .
Diego Costa na Eden Hazard wanatarajiwa kuanza katika mchezo huu baada ya kuanzia bechi katika
mchezo wa kombe la FA dhidi ya Tottenham wikiendi iliyopita
Kiungo wa Southampton Oriel Romeu amereje kwenye kikosi cha timu yake baada ya kufungiwa michezo miwili iliyopita, Sam McQueen is ataukosa mchezo huo akisumbuliwa na
maumivu.
Chelsea wanaongoza ligi kwa alama 75
wakiwa wamecheza michezo 32 wakifuatiwn na Tottenham
wenye alama 71 kwa michezo 32.

Chapisha Maoni

 
Top