0

Bocco ametamba kuwa nilazima waifunge Simba Jumamosi katika mechi ya nusu fainali ya Kombe
la FAMSHAMBULIAJI wa Azam FC , John Bocco ametamba kuwa nilazima waifunge Simba
Jumamosi, katika mechi ya nusu fainali ya Kombe la FA itakayopigwa uwanja wa Taifa Dar es Salaam.
Bocco ameiambia Goal , wamejipanga vyema kwa
ajili ya mchezo huo na wana uhakika wataendeleza rekodi yao nzuri mbele ya timu hiyo ya msimbaza.
“Tumejipanga vizuri hatuna presha kwasababu siyo mara ya kwanza kucheza na Simba na kitu
kizuri tumekuwa tukiwafunga hilo halina ubishi,”amesema Bocco.
Nahodha huyo amesema wanataka kushinda mchezo huo kwasababu ndiyo nafasi pekee kwao
ya kushiriki michuano ya kimataifa hivyo hawatokuwa tayari kuona wanapoteza mchezo huo.
Amesema anatambua kuwa mchezo utakuwa mgumu kwa sababu Simba nao wamejipanga vizuri na hawatokubali kufungwa kwa mara ya tatu lakini bado anaipa nafasi timu yake ya Azam kuibuka na ushindi.
“Unajua hii ni mechi ya kimataifa hivyo hata uchezaji wetu utakuwa ni watofauti na mechi zilizopita na tunafahamu hii ndiyo tiketi yetu
endapo tutafanya vibaya msimu ujao tutabaki humu humu ndani na kitu hicho hatukitaki,’amesema Bocco.
Bocco ndiyo mshambuliaji anayeongoza kuzifunga timu za Simba na Yanga na mara ya
mwisho kukutana na Simba yeye ndiyo alifunga bao kabla ya kuumia dakika chache baadaye na
kutoka nje.


Chapisha Maoni

 
Top