Klabu ya Chelsea The Blues wameendelea na wimbi la ushindi katika vita ya kuwania ubingwa
ligi kuu ya England baada ya kuichapa Southampton kwa 4-2.
Nyota wa timu hiyo Eden Hazard alianza kuiandikia timu yake bao la kuongoza katika dakika ya 5 ya
mchezo , katika dakika ya 45 ya kipindi cha kwanza beki Gary Cahill akafunga bao la pili.
Katika kipindi cha pili mshambuliaji mahiri wa Chelsea diego Costa akaongeza mabao mawili, mabao ya Southampton yalifungwa na kiungo Oriol Romeu na beki Ryan Bertrand.
Chelsea wanaendelea kuongoza ligi wakiwa na alama 78 wakiwa wamecheza michezo 33 huku
Tottenham ikiwa katika nafasi ya pili kwa alama 71 na wakiwa nyuma ya Chelsea kwa mchezo mmoja.
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni (Atom)
Chapisha Maoni