0

Mkuu wa Kitengo cha Habari na
Mawasiliano chs klabu ya Simba Haji Sunday Manara, amesema kuwa anaendelea na majukumu yake ya usemaji wa klabu hiyo kwa kuwa hajapokea barua rasmi kutoka kwa Shirikisho la Soka Nchini (TFF), ya kumfungia kuendelea na kazi yake.
Manara amesema kuwa ataendelea
kupiga kazi huku akisubiri barua ya
maandishi kutoka TFF kama taratibu zilivyo.
Barua rasmi -Mimi naendelea na majukumu yangu,
sijapata barua ,bado naisubiri itakapofika basi nitaacha kwa muda
kazi yangu na kujua nini kinafuata"
amesema Manara.
Manara amesema anaisubiri Barua
hiyo ili pia apate kujua Makosa
aliyopatikana nayo na kujua namna
anavyoweza kuanza harakati za
Kukata Rufaa.
-TFF Sijui wanaogopa nini kunipa hiyo Barua, wakinipa nitajua nimefungiwa kwa Makosa gani ili sasa nianze taratibu za kukataa rufaa, wanalichelewesha Hili jambo wenyewe lingekuwa limekwishakamilika mpaka
hivi sasa" Aliongeza.
Jumapili Manara alifungiwa Jumapili kwa Makosa Matatu Ambapo moja wapo
lilikuwa ni kueneza Ukabila kwa
kusema wazi wazi makabila Ya
Viongozi wa juu wa TFF jambo ambalo ni kinyume na kanuni za Shirikisho hilo.


Chapisha Maoni

 
Top