0
Uongozi wa klabu ya Mbao FC
Umekataa kuthibitisha kuwa Kocha
wao Mkuu Ndairagije Etienne anaweza
kuondoka klabuni hapo Mwishoni
mwa Msimu huu baada ya Kupata ofa
nzuri kutoka Mbeya City FC.
Katibu Mkuu wa Klabu ya Mbao
Richard Athanas amesema hawajapata
ombi lolote kutoka kwa Kocha
Ndairagije la kutaka kuondoka au
klabu nyingine yoyote Ya Kumtaka
Kocha huyo Raia wa Burundi.
-Hata sisi hizo Taarifa tunaziona tu
kwenye Mitandao bado hatujapata
nafasi ya mazungumzo kutoka Klabu
yoyote tunaamini kocha Ndairagije
bado Yupo nasi" Athanas Alisema.
Katibu Athanas Amesema
wanachoamini wao ni Kwamba Kocha
Ndairagije Bado ana mkataba na
wanachotazama sasa Ni namna ya
Kuweza kumaliza ligi katika nafasi
nzuri ili wasishuke Daraja.
Mkataba wa Mwaka mmoja.
-Kocha wetu Bado anamkataba na sisi
japokuwa alikuwa na mkataba wa
Mwaka mmoja Lakini Bado
haujamalizika, na lengo Letu ni
kuhakikisha tunamaliza msimu huu
vizuri" Alisema.
Aidha Athanas aliweka bayana kuwa
kama atapenda kuondoka hawawezi
kumzuia Kwani Wanaamini kazi ya
Ukocha ni Kama Ya mchezaji kila siku
utafuta pale Ambapo kuna Malisho
mazuri.
Taarifa za Ndani.
Kwa Taarifa za ndani zinasema Kocha
Ndairagije mwenyewe ameomba
kujiunga na Mbeya City ili kurithi
mikoba Ya kocha Mmalawi Kinah Phiri
ambaye amekuwa na msimu mbaya
na kikosi hicho cha Kizazi Kipya.

Chapisha Maoni

 
Top