Chipukizi Kylian Mbappe alifunga bao la ushindi na kuwawezesha Monaco kulaza Lyon na kurejea
kileleni mwa Ligi Kuu ya Ufaransa, Ligue 1 mnamo Jumapili.
Radamel Falcao alikuwa amefungia wageni hao bao la kwanza lakini likakombolewa na Lucas Tousart
aliyefungia Lyon bao kwa kichwa.
Lakini Mbappe, 18, alifunga bao lake la 13 ligini msimu huu na kuwaongezea Monaco matumaini
ya kushinda taji lao la kwanza la ligi tangu 2000.
Monaco wanatoshana nguvu kwa alama na Paris St-Germain, lakini wako mbele kwa mabao.
Aidha, wana mechi moja hawajacheza.
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni (Atom)
Chapisha Maoni