0
Kampuni ya Bahati Nasibu ya
SportPesa imeingia mkataba wa Miaka
Mitano wenye Thamani ya Shilingi
Bilioni 4 na Klabu ya Simba ya Jijini
Dar es Salaam.
Udhamini huo ambao umetangazwa
wakati wa Mapumziko kwenye
mchezo wa Ligi Kuu Soka Tanzania
Bara Kati ya Simba na Stand United,
umeifanya Simba kuanza Rasmi kuvaa
Jezi zenye nembo ya Mdhamini wao
mpya katika kipindi cha pili.
Mchanganuo.
Mchanganuo wa mkataba huo
unaonesha kwamba Simba watalipwa
zaidi ya Shilingi Milioni 74.5 Kwa
Mwezi Huku pia wakitarajia kupokea
Milioni 880 kwa Mwaka.
Aidha udhamini huo umetangazwa
mbele ya Mashabiki wa Soka ambapo
Rais wa Klabu hiyo Evans Eveva
alikabidhiwa Jezi na Mkurugenzi wa
SportPesa Tanzania Pavel.
Hii Inakuwa Timu ya Kwanza kuramba
Pesa za SportPesa ambapo Vilabu
vingine vinavyotarajiwa kupokea
udhamini huo ni Yanga SC pamoja na
Singida United.

Chapisha Maoni

 
Top