kujiiamarisha kuelekea ligi kuu soka
Tanzania bara ambapo tayari
imekamilisha Usajili wa Kiungo
Mkabaji wa Tusker FC na Timu ya
Taifa ya Uganda Shafiki Batambuze
kwa mkataba wa Miaka miwili.
Akithibitisha taarifa za kumnasa
Kiungo huyo Katibu mkuu wa Singida
United Abdulrahaman Sima lengo lao
ni kuhakikisha wanajenga kikosi bora
kwa ajili ya misimu miwili ijayo.
-Sisi wachezaji wetu wote wa nje
tunawapa mikataba ya miaka miwili
miwili, tunataka tutengeneze timu
ambayo itakaa pamoja kwa muda wa
miaka miwili ijayo, ili tuitengeneze na
iwe timu bora’ Alisema Sima.
Kuhusu mazungumzo na Klabu ya
Tusker inayoshiriki ligi kuu ya Nchini
Kenya ya kumuachia Kiungo huyo,
Sima amesema tayari wamefikia
makubaliano na Klabu hiyo na
kwamba Bantambuze atajiunga na
Singida United pindi ambapo Mwalimu
atakiita kikosi kwa ajili ya kambi
baadae mwezi ujao.
-Sisi kambi bado hatujaanza na pia
bado hatujaanza kuita wachezaji wetu,
ila tunatarajia atajiunga na kikosi pindi
tu tutakapoanza kambi yetu Juni 12
mwaka huu, na tayari tumewalipa
nusu ya Pesa ya makubaliano Tusker
hivyo hatuna wasiwasi kabisa na
kujiunga kwa Batambuze’ Alisema.
Batambuze ni miongoni mwa
wachezaji waliowika sana na Tusker
msimu uliopita ambapo mwezi
Novemba alichaguliwa kuwa mchezaji
bora baada ya Mabao yake kuisaidia
Timu ya Tusker kutwaa taji la Ligi kuu
nchini Kenya.
Anakuwa wanne.
Tayari Singida United wamekwisha
kamilisha usajili wa Wachezaji watatu
wakimataifa kutoka Zimbabwe ambao
ni Elisha Muroiwa, Wisdon
Musa na Tafadzwa Kutinyu, hivyo
kukamilisha usajili wa Shafik
Batambuze kunafanya kuwa na
wachezaji wanne wa Kigeni Mpaka
sasa.
Chapisha Maoni