kuweka heshima katika mchezo wa
Ijumaa hii dhidi ya Toto Africans
kwani hawapo katika mbio za Ubingwa
msimu huu, na hawatacheza chini ya
Kiwango ukizingatia kwamba Hawana
cha kupoteza.
Msemaji wa Klabu ya Azam Jaffary Idd
Maganga amesema wanatambua kuwa
Toto Africans wanapambana
kutoshuka daraja, na hivyo
wanatarajia upinzani mkali lakini
furaha yao itakuwa ni kuona Azam
Ikishinda na kupata alama Tatu
muhimu.
-Tunafahamu kwamba Toto ni Timu
nzuri na ipo muda mrefu kwenye ligi,
lakini sisi tumekamilika ukiondoa
Yahya timu yote ipo fit, na wapo tayari
kupambana kupata ushindi, mchezo
wa mpira siku zote furaha ni kushinda
kama wewe unataka kushuka
utashuka pekee yako, kushinda ni
heshima katika Timu’ Alisema.
Mzunguko wa Kwanza.
Ikumbukwe kwamba katika Mzunguko
wa Kwanza uliofanyika Novemba 2,
mwaka jana Azam FC waliibuka na
ushindi wa Bao 1-0 mchezo ambao
ulifanyika kwenye uwanja wa CCM
Kirumba Jijini Mwanza huku bao
pekee likifungwa na Shaban Idd
Chilunda.
Chapisha Maoni