Jenerali Sejusa aliyeitoroka uagnda baada ya kutofautiana na rais Musevenei hadharani
Mwanajeshi wa Uganda ambaye alitofautiana hadharani wa rais nchi hiyo Yoweri Museveni mwaka uliopita amerejea nchini Uganda bila
kutarajiwa kutoka nchini Uingereza ambapo alikuwa amekimbilia uhamishoni.
Jenerali David Sejusa aliitoroka Uganda baada ya kumshutumu rais Museveni kwa kujaribu kubuni familia ya kifalme akitaka kumkabithi uongozi mwanawe wa kiume.
Sejusa pia alidai kuwa kulikuwa na njama ya kuwaua watu fulani katika serikali na jeshini ambao walikuwa wakipinga mpango huo.
Rais Museveni anayedaiwa kumtayarisha mwanawe ili kuchukua utawala wa Uganda
Alipowasili mjini kampala Jenerali Sejuse alikutana na mkuu wa ujajusi ambapo pia aliwambia waandishi wa habari kuwa rais Museveni alifahamu
kuhusu kurejea kwake.

Chapisha Maoni