0
Wapiganaji wazidi kushambuliana nchini Libya tangu kuanguka kwa utawala wa Muamar Gadaffi Shambulizi lililolenga kituo muhimu cha mafuta mashariki mwa Libya halikufua dafu kutokana na
mashambulizi ya angani yaliotekelezwa na vikosi vya serikali vinavyotambuliwa kimataifa.

Kamanda mmoja wa jeshi la wanahewa anasema kuwa mashambulizi ya angani yaliwalenga watu wenye silaha waliokuwa wakisonga mbele katika
kituo cha mafuta cha Al-Sidra ambapo watu wengi waliuawa.

Zaidi ya miaka mitatu tangu kuanguka kwa utawala wa kanali Muamar Gadaffi serikali hasimu bado zinapigania madaraka nchini Libya.






Chanzo BBC

Chapisha Maoni

 
Top