na Michezo, Mhe. Dkt. Harrison G.
Mwakyembe (Mb) tarehe 20 April,
2017 amekutana na uongozi wa Klabu
ya Simba ukiongozwa na Rais wake
Bw. Evans Aveva, kwenye ofisi ya
Wizara, hiyo Mjini Dodoma.
Uongozi wa Simba uliitikia wito wa
Mhe. Mwakyembe wa kukutana na
kujadili masuala mbalimbali ya mpira
wa miguu zikiwemo fursa na
changamoto katika mabadiliko na
maendeleo ya uendeshaji wa timu.
Kikao hiko pia kilihudhuriwa na Katibu
Mkuu wa Wizara, Mkurugenzi wa
Michezo wa Wizara, Katibu Mkuu wa
BMT na Msajili wa Vilabu na Vyama.
Mhe. Mwakyembe alipokea maoni ya
Uongozi wa Simba na kuushauri
kuendelea kutoa ushirikiano na wadau
wa mpira wa miguu.
Mabadiliko
Kikao hicho kimetajwa kuwa ni moja
kati ya hatua za kuelekea katika Mpira
wa Kisasa kwa kuwa na mabadiliko ya
Uendeshaji na timu, Ambapo klabu ya
Simba ilikuwa katika harakati za
kubadilisha Katiba ya kuelekea
Mabadiliko hayo Kabla ya zoezi hilo
kukwamishwa na Serikali.
Chapisha Maoni