Nusu fainali ya pili katika kombe la chama chà soka nchini England maarufu kama kombe la FA imechezwa leo baada ya ile ya mwanzo jana ambapo Chelsea waliifunga Tottenham bao 4-2.
Arsenal leo ilitinga fainali ya michuano hiyo mikongwe katika ngazi ya klabu duniani ikiifunga Manchester City bao 2-1.
Sergio Aguero alitangulia kuipatia Man City bao la kwanza dakika ya 62 kabla ya beki Nacho Monreal dakika 10 badae na kufanya mchezo huo kumalizika kwa sare ya bao 1-1 na ndipo
zikaongezwa dakika 30.
Alexis Sanchez ndiye aliyewapeleka Arsenal fainali akifunga bao la ushindi dakika ya 101 baada ya kazi nzuri ya Danny Welbeck na kufanya dakika
120 kumalizika kwa ushindi kwa Arsenal ambao sasa wanatinga fainali wakìtarajiwa kukutana na
Chelsea.
Chapisha Maoni