Mechi mbili za ligi kuu ya England zimechezwa leo katika viwanja viwili nchini humo ambapo Manchester United na Liverpool zote zilikua uwanjani.
Manchester United ikisafiri mpaka uwanja wa Turf Mor iliwavaa wenyeji Burnley na kufanikiwa
kuibuka na ushindi wa bao 2-0.
Magoli ya Manchester United yalifungws yote kipindi cha kwanza na Antony Martial na nahodha Wayne Rooney.
Katika mechi nyingine Liverpool wameendeleza uteja kwa Crystal Palace baada ya kufungwa bao
2-1.
Philip Coutinho alitangulia kuifungia Liverpool bao Lakini Christian Benteke akaibuka shujaa kwa Crystal Palace baada ya kufunga bao la
kusawazisha na lile la ushindi.
Mechi zingine za ligi hiyo zitachezwa Jumanne, Jumatano na Alhamisi wiki hii.
Chapisha Maoni